Home Habari YANGA, SIMBA RASMI UWANJA WA TAIFA

YANGA, SIMBA RASMI UWANJA WA TAIFA

3073
0
SHARE

Na Ezekiel Tendwa

KILIO cha timu za Simba na Yanga kucheza Uwanja wa Taifa mchezo wao wa Jumamosi Ijayo kimesikiwa, baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuthibitisha rasmi kwamba kipute hicho kitachezwa hapo.

Awali Serikali ilisema mchezo huo uhamishwe na kuchezwa kwingine kutokana na Uwanja huo kuwa kwenye matengenezo, lakini sasa TFF wamesema wamezungumza na Serikali na kukubaliana kuutumia.

Yanga, ambao ni mwenyeji wa mchezo huo, walitaka upelekwe Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, baada ya Serikali kudai Uwanja wa Taifa hautatumika na Bodi ya Ligi wakaiambia Yanga uchezwe Uwanja wa Uhuru na sasa ni Taifa.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, ameliambia DIMBA kwamba, mchezo huo sasa ni rasmi utachezwa Uwanja wa Taifa, baada ya kufanya makubaliano na Serikali.

Hiyo inamaanisha kwamba, ombi la timu hizo limekubalika baada ya kuhofia kwamba Uwanja wa Uhuru, hautatosha idadi ya mashabiki ambao wanasema wanaweza wakawa wengi kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here