Home Habari Yanga wapata mrithi wa Gadiel

Yanga wapata mrithi wa Gadiel

0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kutokea vuta nikuvute kuhusu usajili wa beki wa Yanga, Gadiel Michael, mabosi wa klabu hiyo wamekaa tayari kuhakikisha wanabandika chumba kingine hatari kitakachoziba pengo lake.

Anayetajwa kumrithi Gadiel waliyemsajili akitokea katika klabu ya Azam FC ni beki kisiki wa timu ya taifa ya Zanzibar, Muharami Salum ‘Marcelo’.

Marcelo anayedaiwa kusajiliwa na Singida United kwa mkataba wa miaka mitatu, sasa anaelekea kubadilishiwa upepo ili akafanye kazi katika mabingwa hao wa kihistoria, Yanga.       

Habari za uhakika zilizolifikia DIMBA zinasema, beki huyo ametimia viwango na amepewa sifa zote za kupiga mzigo zaidi ya ule aliokuwa akiupiga Gadiel.

“Tayari uongozi wa Yanga umeongea na bosi wa Singida United, Mwiguli Nchemba, ikiwezekana warudishiwe fedha zao za usajili wa huyo mchezaji,” alisema mtoa taarifa hizi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Dkt Mshindo Msolla, mjadala wa Gadiel kwasasa umefungwa ili kumwachia aamue anavyodhani inafaa.

Kwa upande wa kocha wake, Mwinyi Zahera, amewataka mabosi wake kutombembeleza beki huyo na badala yake waangalie wachezaji wengine watakaokua na manufaa na mapenzi na timu yao.

Awali Yanga kupitia kwa mmoja wa viongozi wake walisafiri hadi nchini Misri wakati Taifa Stars ikiendelea na michuano ya Kombe la Afrika na kumpelekea mkataba mchezaji huyo lakini akawawekea ngumu akidai kutosaini hadi atakapokabidhiwa dau analohitaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here