Home Habari YANGA YAFANYA BONGE LA ‘SURPRISE’

YANGA YAFANYA BONGE LA ‘SURPRISE’

360
1
SHARE

NA JESSICA NANGAWE,

YANGA wamesikia fujo za watani wao, Simba walizoanza nazo kwenye usajili wao msimu huu na kutafakari kwa kina, lakini wenyewe wameamua kufanya usajili wao kwa siri kubwa, huku mpaka sasa wakishindwa kuonyesha dalili zozote za wachezaji wanaowataka msimu ujao.

Wakati kukiwa na tetesi kuwa baadhi ya nyota huenda wakatua Msimbazi, kwa upande wa wapinzani wao mambo bado hayajawekwa hadharani mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, watafanya usajili kulingana na ripoti ya Kocha Mkuu, George Lwandamina, lakini kwa sasa bado wanafanyia kazi ripoti hiyo.

Alisema usajili wao utazingatia vigezo vilivyotolewa na kocha huyo na wakati utakapokuwa tayari wataweka wazi usajili wao.

“Kwa sasa tunapitia mapendekezo ya kocha Lwandamina na kuangalia ni jinsi gani tutaongeza wachezaji kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu msimu ujao,” alisisitiza Mkwasa.

Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuachwa na kikosi hicho ni Deus Kaseke, Malimi Busungu, Matheo Antony, Justice Zullu, Ally Mustapha ‘Barthez’.

Wachezaji ambao wanatajwa kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ni Mbaraka Yussuf, Raphael Daud, Ally Nassor ‘Ufudu’ na Yusuph Ndikumana, ambaye pia anatajwa na watani wao, Simba.

Kwa upande wa benchi la ufundi, huenda likawa na marekebisho ambapo Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, anatajwa kutua ndani ya kikosi hicho, huku kocha msaidizi, Juma Mwambusi akitarajiwa kuondoka sambamba na kocha wa makipa, Juma Pondamali.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here