Home Habari Yanga yaishika pabaya Al Ahly

Yanga yaishika pabaya Al Ahly

788
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

ACHANA na Yanga bwana.

Kwa kuinyuka APR ya Rwanda nyumbani kwao kwa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita,  tayari wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika wamepata kiburi cha kusonga mbele raundi ya pili kabla ya mechi ya marudiano.

3-201Kwa kuamini kazi ya kuitoa APR imekwisha, tayari Yanga imeishika pabaya timu ya Al Ahly ya Misri ambayo sasa imeelekeza vita huko na tayari imeshanasa siri muhimu zitakazoisaidia timu hiyo kushinda pindi zitakapokutana.

Itakumbukwa Yanga haina rekodi nzuri ya ushindi inapokutana na timu za Waarabu, lakini safari hii kwa kujua wanaweza kukutana na Al Ahly ambayo iliwatoa mwaka juzi, tayari wameshaisoma timu hiyo ili kuhakikisha wanavunja mwiko endapo zitafanikiwa kukutana.

Jumamosi iliyopita Yanga ilianza raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa kuichapa APR ya Rwanda mabao 2-1 jijini Kigali na timu hizo zitarudiana Jumamosi hii Uwanja wa Taifa jijini na timu hiyo ya Jangwani inaamini kazi hiyo imekwisha na akili yao ni kwa Al Ahly tu.

Yanga imeamua kuifungia kazi mapema Al Ahly baada ya Waarabu hao kuelekea kufanikiwa nafasi ya kucheza nao baada ya kutoka suluhu ugenini ilipocheza na Libolo FC ya Angola.

Matokeo hayo yanaipa nafasi kubwa timu hiyo kusonga kwa vile mechi ya marudiano na Waangola hao itachewa nchini Misri.

Uongozi wa Yanga na mashabiki wa timu hiyo wanaamini kwa mbinu chafu za Al Ahly ndani na nje ya uwanja wakiwa nyumbani haziwezi kuipa nafasi FC Libolo kushinda na hivyo kuwa na uhakika wa kucheza na Waarabu hao hatua inayofuata.

Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa kutambua wanaweza kukutana na Al Ahly tayari inaufanyia kazi mfumo wa 4-2-3-1 unaotumiwa na timu hiyo inapocheza ugenini.

“Al Ahly wakiwa ugenini wanapenda kutumia mfumo huo ambao ndio uliowawezesha kupata suluhu dhidi ya Libolo ambao unaaminika kama ni mbinu ya kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza,” alisema mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi Yanga ambaye hakupenda kutajwa kwa vile si msemaji.

Alisema maana kubwa ya Waarabu hao kutumia mfumo huo ni kuhakikisha wanapata matokeo yoyote ya sare ugenini wakiamini kuwa lazima waibuke na ushindi watakapocheza uwanja wao wa nyumbani.

Hiyo ni moja ya mbinu ambazo Yanga wameanza kuzigundua na kama Waarabu hao watapenya mbele ya Libolo ni wazi watakabiliana na muziki mnene wa Wanajangwani hao.

Ligi ya Misri

Msimu uliopita Waarabu hao walimaliza ligi wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 79, nyuma ya mabingwa Zamaleck waliomaliza ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 87.

Katika ligi ya msimu huu, Al Ahly wanaongoza wakiwa na jumla ya pointi 47 katika michezo 21 waliyokwisha cheza mpaka sasa wakifuatiwa na Zamaleck wenye pointi 41.

Straika wa kuchungwa

Katika kikosi cha Waarabu hao yupo mkali wao wa mabao anayejulikana kwa jila la Malick Evouna ambaye katika mchezo dhidi ya Libolo ndiye aliyesimama kama mshambuliaji wa mwisho.

Katika msimamo wa wafungaji msimu huu straika huyo anashika nafasi ya saba akiwa na mabao saba sawa na winga wa kulia wa kikosi hicho, Abdallah Said, mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu.

Kauli ya Yanga

Wakiwazungumzia Waarabu hao, Yanga wamesema wapo tayari kupambana nao kwani wana uhakika kikosi chao kimekamilika kila idara, ndiyo maana wamekuwa wakipata ushindi kwa kila timu wanayokutana nayo msimu huu.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema licha ya kwamba Waarabu hao waliwatoa mwaka juzi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, safari hii hawatapata ushindi kama walivyozoea.

“Kama ndio tutakutana nao sisi tunawakaribisha kwa mikono miwili na niwaambie tu kwamba Yanga ilivyo sasa ni kupiga tu bila kuangalia tunayekutana naye,” alisema.

DIMBA lilipotaka kujua kama Libolo watawatoa Waarabu hao na kuvaana na Yanga, Muro alisema Yanga kwa sasa haikamatiki na kama hao Libolo waliwafunga Simba hiyo haiwatishi na badala yake wamejipanga huku akisisitiza ‘sisi tunapiga tu’.

Mashushushu kuwapeleleza Al Ahly

Dimba lilitaka kujua endapo Yanga nao watatuma mashushushu wao kwa ajili ya kwenda kuipeleleza Al Ahly katika mchezo wake na FC Libolo ambapo Muro alisema jambo hilo ni siri kubwa.

Licha ya kwamba msemaji huyo ameshindwa kuweka bayana juu ya jambo hilo, DIMBA linafahamu kuwa Wanajangwani hao watatuma mtu mmoja makini ili kwenda kuwasoma wapinzani wao hao.

Kama Yanga watafanikiwa kukutana na Waarabu hao watataka kumalizia hasira zao za msimu uliopita walipotolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti ambapo Said Bahanuzi ndiye aliyekosa penalti ya mwisho ambayo ingeiandikia historia timu hiyo kwa mara ya kwanza kuitoa timu ya Kaskazini mwa Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here