Home Habari YANGA YAMTIBUA LECHANTRE

YANGA YAMTIBUA LECHANTRE

6889
0
SHARE
NA SAADA SALIM

KUMBE si Wabongo tu, hata Wazungu wanatibuka pindi wanaposikia jambo fulani likijadiliwa mahali pasipohusika.

Hiyo ilitokea jana kwenye ukumbi wa Makao wa Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), pale kocha mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, alipoamua kuondoka ukumbini humo mara baada ya kusikia jina la mahasimu wao Yanga likitajwa kwenye mkutano wao.

Pierre alikuwa TFF pamoja na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara na Ofisa Habari wa TFF, Clifford, ndipo kuzungumzia maandalizi ya mchezo kati ya Simba na Al Masry ya Misri, unaotarajiwa kupigwa leo Uwanja wa Taifa.

Ilikuwa ni katika kipindi cha maswali na majibu, mara baada ya kocha huyo kumaliza kuzungumzia maandalizi yake ya mchezo dhidi ya Al Masry, ndipo mwandishi mmoja akawauliza Manara na Ndimbo juu ya kitendo cha klabu ya Yanga juzi kutojumuika na wapinzani wao Township Rollers katika kikao cha pamoja kama ilivyo kwa Simba.

Lechantre aliposikia neno la Yanga, alinyanyuka na kusema hafahamu Kiswahili, lakini amelisikia jina la hasimu wake wakati yupo katika maandalizi ya mchezo wa Al Masry.

Licha ya kitendo hicho, Lechantre alitoka kabisa ukumbini huku baadhi ya waandishi na wadau mbalimbali wakiamini kuwa huenda ni tabia yake ya kujali muda ndio maana ameamua kutoka ukumbini kuwahi majukumu mengine.

Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kuzungumzia hilo zaidi ya watu mbalimbali waliokuwepo hapo kubaki wakiwa wamepigwa na butwaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here