SHARE

MWANVITA MTANDA NA WINFRIDA MTOI

YANGA haitaki kulaza damu bali kuhakikisha wanarejea uwanjani wakiwa na kasi yao ile ile ya soka la burudani baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Luc Eymael, kubuni njia mpya kuendelea na program zake.

Njia ambayo kocha huyo amekuja nayo, ni kusimamia mazoezi ya program alizowapa wachezaji wake kupitia mtandao, akiwaunganisha kwa pamoja na kuwafuatilia kila siku.
Hiyo imetokana na Ligi Kuu Tanzania Bara kusimama kutokana na agizo la Serikali ili kuepuka mikusanyiko inayoweza kusababisha kusambaa kwa virusi ya ugonjwa wa Corona.

Hali hiyo imezifanya timu nyingi duniani kuvunja kambi na wachezaji kurejea nyumbani, hivyo baadhi ya makocha na nyota wa kigeni wamerudi katika nchi zao akiwamo wa Yanga.
Eymael kwa sasa yupo nchini kwao Ubelgiji, alikwenda kwa mapumziko na familia yake, huku akisikilizia ni lini ligi hiyo itarejea baada ya siku 30 zilizotolewa kumalizika.

Kocha huyo amebaini kuwa wachezaji hawatakiwi kuachwa wenyewe, bali usimamizi unahitajika ili kufanya kile anachotaka na kuwaweka fiti, hivyo kuwanoa katika mtandao itakuwa ni njia sahihi kwa sababu kila mmoja anamiliki simu ya kisasa.
Kupitia njia hiyo, wanaweza kufanya hata vikao vyao vya kawaida vya kupeana mikakati kama inavyofanyika katika klabu nyingi Ulaya.
Ikumbukwe kuwa wakati ligi hiyo inasimama, Yanga ilikuwa inapigania kukaa katika nafasi ya pili na kikosi chake kilikuwa kimeanza kupamba moto.

Katika msimamo wa Ligi, inashika nafasi ya tatu na pointi 51, baada ya kucheza mechi 27, nyuma ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili na alama 54, ikishuka dimbani mara 54.
Lengo lingine la Eymael kuendelea kukiweka kikosi chake fiti na kujiandaa na mechi za robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) ambayo ndiyo pekee yenye uhakika wa kuwapeleka kimataifa.

Akizungumzia program hiyo ya mtandao, Eymael, alisema ameunda kundi maalum la WhatsApp linalotumika kuwapa maelekezo nyota wake kila siku asubuhi.
Alisema, amewambia lazima wakimbie hata katika eneo la nyumbani na kufanya mazoezi madogomado kila siku asubuhi na jioni, ili miili yao isilemae kwa kipindi hiki.

Mwili ambao umezoea mazoezi hauwezi kukaa bure mwezi mzima, kwa kufanya hivyo naamani watakuwa salama mpaka tukikutana.
Natambua tabia wachezaji yani ni kama watoto endapo sitakuwa makini wanaweza kujisahau na wakirudi kazi ikawa ngumu zaidi, ni juku langu kuzingatia hata kama tuko mbali mbali kwa muda huu,îalisema Eymael.

Hata hivyo Mbelgiji huyo alisema, kutokana na maambukizi ya Virusi hatari vya Corona, amewazuia nyota wake kuto kwenda kwenye kumbi za starehe.
Alisema kati ya mazoezi anayowaelekeza ni kukimbia hata katika eneo la nyumbani na mengine madogomadogo kila siku mara mbili, asubuhi na jioni.

Nafanya hivi kwa sababu mwili uliozoea mazoezi hauwezikukaa mwezi mzima, ni hatari kwa usalama wa viwango na afya zao.
ìNatambua tabia za wachezaji ni kama watoto wanahitaji kufuatiliwa, endapo nitakaa kimya, watajisahau na kunipa kazi ngumu nitakaporejea,î alisema.

Alisema mipango yake ni kuhakikisha Yanga inashiriki michuano ya Kimataifa, lazima apambane kwa sababu watani wao Simba wanaongoza Ligi.
Yanga ni timu kubwa siwezi kufanya mzaha, pia nataka kulinda kibarua changu, kwa umri wangu natakiwa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu,îalisema Eymael.
Eymael alisema anasisitiza wachezaji hao kubaki nyumbani na kuacha kwenda kumbi za starehe zinazoweza kusababisha kuambukizwa Virusi vya Corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here