Home Habari YANGA YAPORA SIMU ZA WACHEZAJI MBAO

YANGA YAPORA SIMU ZA WACHEZAJI MBAO

1943
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE


WAKATI mechi nyingine yenye mvuto katika michuano ya Ligi Kuu, itakayoikutanisha Yanga na Mbao FC ikitarajiwa kupigwa leo, kambi ya timu hiyo kutoka Mwanza imewekewa ulinzi wa aina yake.

Mbao FC, ambayo kwasasa ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi, ikiwa chini ya vinara, Mtibwa Sugar na Azam FC, itacheza na mabingwa hao wa kihistoria huku ikiwa na kumbukumbu ya kuwafunga watani wao wa jadi, Simba kwa ushindi wa bao 1-0, mechi iliyochezwa Septemba 20 mjini Mwanza.

Ushindi huo dhidi ya Simba na kisha kushinda mechi nyingine tatu umeifanya timu hiyo kuwa tishio miongoni mwa timu za Ligi Kuu msimu huu.

Kabla ya mchezo huo wa leo, timu hiyo ilicheza mechi yake ya nane dhidi ya Costal Union, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Mkwakwani, ambapo Mbao walipoteza mchezo huo kwa kuchapwa bao 1-0.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here