SHARE
Young Killer

NA BEATRICE KAIZA

RAPA mahiri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Erick Msodoki Young Killer amesema, kutokana na changamoto ambazo anakutana nazo kwenye kazi yake ni vema kutembea na mabaunsa.

Akizungumza na DIMBA, Young Killer,alisema, moja ya matukio yanayomlazimu kuwa na walinzi ni lile lililowahi kumpata ambapo alivamiwa jukwaani na shabiki na kusababisha fujo.

ëíMsanii kuwa na mbavu nene yaani walinzi ni sahihi mimi imenitokea nikiwa kwenye shoo mmoja nilivamiwa na shabiki na kuzua taharuki ila mashabiki wote sio wema unakuta wengine wanafanya fujo na kuiba vitu kama saa na cheni kwa sasa siwezi kwenda sehemu bila ya kuwa na baunsa kwa usalama wangu, alisema Young Killer.

Aliongeza kuwa kwa msanii staa kutembea na mabaunsa sio kama ni kosa ila ni katika kujiwekea ulinzi wa mali na usalama wako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here