Home Habari ZAHERA AACHA SUMU YA KUIUA MBAO DAR

ZAHERA AACHA SUMU YA KUIUA MBAO DAR

1536
0
SHARE

CLARA ALPHONCE NA EZEKIEL TENDWA


YANGA wanashuka dimbani leo kuwakabili Mbao FC, bila Kocha wao Mkuu, Mwinyi Zahera, lakini hiyo haitakuwa na madhara yoyote kwa Wanajangwani hao, kwani Mkongo huyo alimwachia msaidizi wake mikoba ya ushindi.

Zahera aliondoka nchini Jumatano ya wiki hii kwenda kwao DR Congo kujiunga na timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya michuano ya Afcon mwakani nchini Cameroon dhidi ya Zimbabwe.

Zahera ndiye kocha msaidizi wa timu hiyo ya Taifa ya Congo, ndiyo maana amewahi mapema ili kuweka mambo sawa kutokana na umuhimu wa kuikabili timu ya Zimbabwe.

Akizungumza na DIMBA, kabla ya kuondoka, Zahera alisema ana imani kwamba Yanga wataibuka na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Mbao, kwani alimuachia msaidizi wake, Noel Mwandila, ‘sumu’ zote za kuwakabili wabishi hao kutoka jijini Mwanza.

“Mimi ni kocha wa Yanga, lakini pia ni  …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here