Home Habari ZAHERA AFUMUA KIKOSI YANGA SC

ZAHERA AFUMUA KIKOSI YANGA SC

2310
0
SHARE

NA SAADA SALIM


BAADA ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ndanda FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ni kama amevurugwa kichwa chake na sasa anataka kufumua kabisa kikosi chake ili kukiunda upya.

Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamecheza michezo 10 mpaka sasa, lakini kinachowauma zaidi ni kutoka sare na Ndanda, tena Uwanja wa Taifa.

Kabla ya mchezo huo dhidi ya Ndanda FC, Yanga walitoka sare dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, huku mingine wakitoa dozi, ndipo wakaja kutibuliwa tena na walima Korosho hao wa mkoani Mtwara.

Hali hiyo ya kutoka sare na Ndanda imewaumiza sana mashabiki wa Yanga, ambao wamefika hatua ya kutaka ufanyike usajili wa nguvu, hasa safu ya ushambuliaji na kuongeza beki mmoja atakayeshirikiana na Kelvin Yondani.

Kilio hicho ni kama kimefika kwa kocha Zahera, ambaye amesema iwe mvua au jua, lazima atafanya usajili wa maana, lengo likiwa ni kufumua kabisa kikosi chake na kukijenga upya kiwe imara zaidi.

ìLazima tufanye usajili, mpaka sasa nafikiria kuongeza wachezaji wanne, beki mmoja, kiungo mmoja na winga, lakini pia kwenye safu ya ushambuliaji nitaongeza mmoja,î alisema.

Zahera alisema wachezaji hao wanatoka nje ya nchi na huenda wengi wao wakatokea nchini Congo, huku ikidaiwa kwamba yupo straika matata anayecheza soka nchini Gabon na beki kutoka Rwanda, ambao tayari wameshaingia kwenye rada zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here