Home Habari ZAHERA AMNG’ANG’ANIA IBRAHIM AJIB YANGA SC

ZAHERA AMNG’ANG’ANIA IBRAHIM AJIB YANGA SC

1773
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE

WAKATI Simba wakijipanga kumrejesha kundini Ibrahim Ajib, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema jambo hilo halitawezekana, kwani mpaka anampa straika huyo kitambaa cha unahodha, anajua mchango wake kikosini.

Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa bilionea wao, Mohamed Dewji ‘Mo’, anahusudu sana uwezo wa Ajib na ameshamuweka kwenye mipango ya kumsajili kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa msimu huu.

Hata hivyo, Zahera amewaambia viongozi wa Yanga wahakikishe kiungo mshambuliaji na nahodha wao huyo, haendi popote, kwani litakuwa kosa kubwa sana kumkosa kwenye timu yao msimu unaokuja.

“Ajib ni mchezaji mzuri sana, sihitaji kumpoteza kabisa, ndiyo maana nasema lazima apewe mkataba mpya mapema, huyu ni hazina kubwa kwenye timu,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samwel Lukumay, ni kama amemshusha presha Zahera, baada ya kusema Ajib hawezi kuondoka kirahisi kwa Wanajangwani hao.

 “Ukiangalia Ajib kaisaidia sana Yanga tangu kusajiliwa kwake, hivyo tupo kwenye mchakato wa kufanya naye mazungumzo kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya,” alisema Lukumay. Huu ni msimu wa pili kwa Ajib kuichezea Yanga akitokea Simba na ameonyesha uwezo mkubwa, ndiyo maana Wekundu hao wa Msimbazi wanataka kumrejesha, huku wapinzani wao wakiweka ngumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here