SHARE

NA JESSCA NANGAWE KOCHA

Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemtazama mpinzani wake, George Lwandamina, na kudai licha ya kuifahamu Yanga nje ndani lakini ni dhahiri hana mipango yoyote ya kuifunga timu yake katika mchezo ujao.

Yanga itakutana na Zesco United ya Zambia mapema mwezi ujao katika mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufanikiwa kusonga mbele kwa kuiondoa Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Zahera alisema kwasasa akili yake ni michezo iliyo mbele yake; Ligi Kuu Tanzania Bara na mchezo wa kimataifa, ambayo yote anahitaji kupata ushindi.

Alisema anatambua kocha wa Zesco, Lwandamina alikua mmoja wa makocha waliowahi kuifundisha Yanga, lakini si kigezo cha kuifahamu vyema timu hiyo kwasababu sasa kikosi hicho kina mabadiliko makubwa ya wachezaji.

“Kuizungumzia Zesco United kwasasa si wakati wake, tunaangalia mechi za ligi iliyo mbele yetu kabla ya mchezo huo, nafahamu Lwandamina alishapita Yanga lakini si kigezo cha kutambua uwezo wetu na mipango yetu,” alisema Zahera.

Lwandamina alikabidhiwa mikoba ya kukifundisha kikosi cha Yanga akitikea Zesco United mwaka 2016 hadi 2018 na kisha kurejea kwa mara nyingine kuinoa timu hiyo ya Zambia.

Miongoni mwa wachezaji waliofundishwa na kocha huyo ambao mpaka sasa wapo ndani ya kikosi cha Yanga ni pamoja na beki Kelvin Yondan, Said Makapu, Juma Abdul, Ramadhan Kabwil pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here