SHARE

Na Lulu Ringo, Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amewataka mashabiki wa timu hiyo kutowatupia lawama wachezaji wake wanapofanya vibaya kwenye mechi kwa kuwa wanafanya mazoezi katika mazingira magumu mno.

Kutokana na hilo kocha huyo amewataka mashabiki hao wajitokeze kwenye mazoezi waone namna vijana wao wanavyofanya mazoezi.

“Wachezaji wangu wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye mazingira magumu kiasi kwamba huwa natokwa na machozi, ndiyo maana natamani mashabiki wa Yanga nao wafike kwenye mazoezi ya timu ili waone mazingira ya timu yao ili wapunguze lawama pindi wanaposhindwa kupata matokeo wanayoyatarajia.

“Mashabiki manaipenda Yanga mnapaswa kutambua kwamba wachezaji wenu wanajitoa kwa hali na mali, licha ya changamoto wanazokutana nazo katika maisha, hakuna mchezaji yeyote duniani anayeweza kuvumilia kama hawa wanavyovumilia,” amesema kocha huyo.

Zahera ameongeza kwamba mashabiki wengi wanataka matokeo mazuri lakini hawafahamu hali za wachezaji wao kiuchumi zikoje.

“Nilichokiona kwa mashabiki wa Tanzania wana maneno sana, wengi wao wanahitaji timu ishinde kwa miujiza, lakini hata hali za wachezaji na familia zao hawazijui. Mashabiki wa Yanga ni wengi wajitokeze kuibea timu yao ili ifanye vizuri zaidi,” amesema Zahera.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here