Home Habari ZAHERA: NITAKUFA NA YANGA

ZAHERA: NITAKUFA NA YANGA

6171
0
SHARE

Lulu Ringo, Dar es salaam

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema hana mpango wa kuondoka klabuni hapo hata kama kuna timu itamuhitaji kwa dau lolote lile.

Zahera amesema hayo baada ya timu ya Builcon kutoka Zambia kuonyesha nia ya kuhitaji huduma yake lakini yeye amesema hayupo tayari kuvunja mkataba wake na Yanga kwa kuwa amejitolea kuifundisha timu hiyo hadi mwisho.

“Hata nipewe dola za marekani 40,000 siwezi kuiacha Yanga kwa kuwa maisha siyo pesa tu, huwa nawaambia wachezaji wangu wavumilie na wapambane katika kila mechi sasa iweje leo niiache Yanga sababu nimepata nafasi nyingine, napenda wachezaji wangu washinde hivyo hata Yanga ikifa nitakufa nayo.

“Mimi familiya yangu haikunifundisha hivyo, mimi si masikini wakukimbilia pesa maisha yangu leo yako vizuri kwa nguvu ya mwenyezi mungu na siyo pesa,” amesema Zahera

Zahera amesaini Yanga kandarasi ya kunoa kikosi hicho kwa miaka miwili akipokea mikoba ya George Lwandanima wa Zambia lakini pia Zahera ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DRC Congo.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here