SHARE

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema sababu kubwa inayoiponza timu yake kushindwa kufunga magoli ni uzembe unaosababishwa na mastraika wake kwa kushindwa kumalizia mashambulizi yanayozalishwa na safu nzima ya ushambuliaji.

Akizungumza jana baada ya mchezo wao dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara, Zahera amesema hayo baada ya timu hiyo kukosa magoli mengi ya wazi kupitia kwa mshambuliaji wake, Haritier Makambo hali iliyosababisha timu hiyo kutoka sare ya goli 1-1, magoli yaliyofungwa na Vitalis Mayanga (Ndanda fc) dakika ya 15 na Jaffar Mohamed (Yanga) dakika ya 24.

“Siwezi kusema tatizo ni safu ya ushambuliaji, mechi nyingi tunazocheza tunatengeneza nafasi za kutosha lakini tunashindwa kufunga, kama alivyofanya makambo leo (jana) kama angekua mama yangu pale angefunga goli kwa Kichwa” alisema Zahera.

Licha ya sare hiyo ya pili kwa Yanga katika uwanja wa Taifa baada ya ile ya 0-0 na Simba Sc, kocha huyo amesema timu yake haijapoteza ujasiri wa kuendelea kusaka ubingwa kwakua hakuna mchezo aliopoteza katika michezo 10 walizocheza.

“hatuwezi kupoteza kujiamini, kwani tumefungwa? Tungekua tumefungwa magoli 6-1 ningesema tumepoteza kujiamini sisi si Barcelona wala PSG, useme hatuwezi kufungwa, tumecheza mechi 10 na hatujafungwa, nimewaambia wachezaji wangu walale vizuri mechi zizayo watashinda,” alisema Zahera.

SHARE
Previous articleHUYO BIEBER MWACHENI TU
Next articleSIMBA SASA NI MOTOO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here