Home Michezo Kimataifa Zidane Zidane: Heshima yake inaweza kushushwa ghafla na Perez

Zidane Zidane: Heshima yake inaweza kushushwa ghafla na Perez

548
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

UKITAJA jina la Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, kama moja ya majina ya watu wanaofanya maamuzi ya kukurupuka bila shaka utakuwa hujakosea kwani amewahi kufanya hivyo.

Hakuna aliyedhani kuwa bosi huyo angemtimua mtu kama Carlo Ancelotti ambaye alikuwa ameshaanza kujenga kikosi kazi, lakini kufumba na kufumbua ikatangazwa kuwa si kocha tena wa Real Madrid.

Tabia ya Perez ni kama ya mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovic ambaye naye uvumilivu kwake si kitu cha muhimu ambapo huwa anachoangalia zaidi ni timu kupata matokeo ya ushindi akidhani kuwa timu nyingine hazitaki ushindi.

Kwa sasa katika kikosi hicho cha Real Madrid kinaongozwa na mchezaji mwenye heshima kubwa Mfaransa Zinedine Zidane, ambaye anakumbukwa sana kutokana na mchango wake aliouonyesha enzi za uchezaji wake.

Hata hivyo, bahati mbaya aliyonayo ni kwamba rais wa timu yake yeye ni dakika mbili mbele, huwa hakawii kumuonyesha mtu mlango wa kutokea hata kama timu haijafanya vibaya na hilo lilijitokeza kwa Ancelotti.

Tabia ya Perez ni kwamba anataka kila akiulizia matokeo aambiwe timu yake imeshinda, hataki kusikia kushindwa kwa namna yoyote ile hata timu ikipata sare kwake ni sawa na kufungwa, hiyo ndiyo tabia ya bosi huyu.

Hatari inayoanza kumnyemelea Zidane ni kwamba kikosi hicho kimefululiza kupata matokeo ya sare kitu ambacho kinaweza kumuathiri mbele ya safari, anaweza akajikuta anaambiwa aanze kufungasha kila kilicho chake na kupisha wengine.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Real Madrid ilijikuta ikipata sare na timu ya Eibar, tena mbaya zaidi ni kwamba walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani na timu ambayo wamekutana nayo ni moja ya timu ambazo zinaonekana kama zisizo na sumu.

Vitu kama hivyo ndivyo ambavyo Perez hataki kuvisikia kabisa. Huwa anawaza kwamba kikosi chake kinao wachezaji wenye majina makubwa duniani kama akina Cristiano Ronaldo na Gareth Bale sasa iweje wapate matokeo mabaya.

Ni kweli kwamba Zidane ni mtu wa heshima ndani ya Madrid, hakuna ubishi enzi za uchezaji wake alionyesha uwezo mkubwa na kukisaidia kikosi hicho kupata makombe mbalimbali lakini kwa nafasi aliyopo anaweza akatumbuliwa mchana kweupe na huyo aliyeshika mpini.

Angalau kitu kinachoendelea kumbeba Zidane kwa sasa ni kwamba hata wapinzani wao wa jadi hawajapata matokeo ya asilimia mia moja, kitu kinachowafanya kushika nafasi ya pili na kama wataendelea kupata matokeo mazuri mechi zijazo watakalia kileleni.

Wapinzani wao Barcelona ambao huwa hawafanyi makosa, msimu huu nao unaonekana si mzuri sana kwani wameshapoteza michezo miwili kati ya saba waliyokwisha kucheza kitu ambacho kinawafanya kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Licha ya kwamba Madrid ya Zidane imetoka sare mara tatu, lakini inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 15 sawa na Atletico Madrid na hicho ndicho angalau kinaendelea kumpa uvumilivu mzee wa maamuzi ya kushtukiza Perez.

Msimu uliopita Zidane ambaye alichukua timu katikati baada ya Rafa Benitez kutimuliwa, alianza kibarua chake kwa kishindo na mwisho wa siku wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Atletico Madrid.

Hata hivyo, yote hayo yanaweza kufutika kwenye kichwa cha Perez kama ataona yale anayoyataka hayatimii. Zidane anatakiwa kutuliza akili yake na kuweka mambo sawa kabla bosi wake hajaangalia wa kuchukua nafasi yake kwani hakawii kufanya hivyo.

Hata hivyo, Zidane ni kocha ambaye wachezaji wanamuelewa, wanajua kwamba ni mtu aliyefanya mambo makubwa enzi zake, hawawezi kumdharau hata kidogo. Yote hayo yanaweza yakamsaidia lakini akiteleza kidogo tu anaweza kupewa mkono wa kwaheri na ile heshima yake ikaporomoka ghafla.

 

Madadi alisema kutokana na vurugu hizo, kamisaa huyo kutoka Afrika Kusini aliomba majina ya walioshambuliwa na akaahidi kuyaweka matukio hayo kwenye ripoti yake lakini majibu yake hayakutoka mpaka sasa.

Katibu Mkuu wa TFF wakati huo, Angetile Osiah, alisema shirikisho liliyapokea matokeo hayo kwa masikitiko kwa sababu  lilifanya juhudi kubwa katika kuhakikisha safari hii timu za vijana zinapata maandalizi bora, lakini juhudi hizo zimekwamishwa na mazingira mabaya kama yalivyoripotiwa na viongozi wa msafara wetu.

Bila kupepesa macho wala kung’ata maneno ni ukweli usiopingika kuwa huu wimbo wa tutajipanga kila timu ikifanya vibaya umetukinai Watanzania na wapenda soka kwa ujumla, hasa wenye kiu ya maendeleo.

Baada ya kuondolewa kwenye mashindano hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, shirikisho hilo limesema kuwa sasa akili zinaelekezwa kwenye mashindano yajayo kwa timu ya vijana chini ya miaka 20 ambapo wachezaji hawa watakuwa kwenye kikosi hicho.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here