Home Michezo Kimataifa ZLATAN AWACHIMBA BITI WENZAKE

ZLATAN AWACHIMBA BITI WENZAKE

457
0
SHARE

MANCHESTER, England

ZLATAN Ibrahimovic amevunja ukimya na kuwaambia wachezaji wenzake kuwa wanapaswa kubadilika haraka iwezekanavyo, la sivyo safari ya Manchester United kwenye Premier League, itabaki kuwa kichekesho tu.

United wako nyuma kwa pointi 13 na vinara wa ligi Chelsea, baada ya kupata mfululizo wa matokeo mabovu, ikiwemo sare 6 kwenye mechi 8 za hivi karibuni.

Vijana hawa wa Jose Mourinho wanashika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa EPL na Ibrahimovic anaamini mchezo wa leo dhidi ya Tottenham ni wa kufa na kupona kwao ikiwa kweli wanataka kumaliza ndani ya ‘top 4’ msimu huu.

United mpaka sasa kwenye Premier League wamefunga jumla ya mabao 19, wakizidiwa na na West Brom na Crystal Palace

“Tunatakiwa kushinda kila mchezo tutakaocheza,” alisema Ibrahimovic. “Kama tunaweza kutengeneza nafasi nyingi basi hatuna sababu ya kukosa matokeo.

“Ni muhimu kwetu kupata pointi tatu bila kujali tumezipata kwa matokeo ya ushindi wa bao 1-0, au 4-0.

“Nafikiri tunacheza soka safi kuliko klabu zote na tuna kikosi imara, tunadaiwa matokeo sasa na mashabiki wetu.

“Tumekosa bahati kwenye michezo baadhi tuliyocheza, tumefanya makosa madogo yaliotugharimu lakini bado tumeendelea kuwa bora uwanjani. Tunatakiwa kubadilika haraka na kupata matokeo ili kurudi kwenye nafasi ya kumaliza kwenye nafasi nzuri mwisho wa msimu,” alisema Ibrahimovic.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here