SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kutambulishwa kwenye lebo ya Wcb mwanadada Zuchu amekiri kuwa sehemu ya ndoto yake imetimia na anachotamani kwa sasa ni kuiheshimu na kuipigania.

Zuchu ambaye tayari kaachia Ep yake yenye nyimbo saba kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Wana’.

Akizungumza na DIMBA, Zuchu alisema ndoto yake kubwa ilikua kufanya kazi chini ya wasanii wakubwa kama Diamond na anashukuru hilo umefanikiwa.

‘Kila kitu ni mipango ya Mungu..nilitamani sana kufika hapa nilipo..Mungu amesikia haja yangu..kwa sasa napigana kuisimamia ndoto yangu na kuiheshimu’Alisema.

Aidha amekiri kuwa mama yake Khadija Kopa anechangia kwa kiasi kikubwa kutimiza ndoto zake za kuwa mwanamuziki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here