SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

NYOTA wa kimataifa wa Yanga, Justine Zulu, anaamini makali walioanza nayo michuano ya Ligi ya Mbingwa dhidi ya Ngaya mwishoni mwa wiki ikiwamo yeye mwenyewe kufunga bao, ni mwanzo tu wa safari ndefu waliyonayo.

Katika mchezo huo uliopigwa Jumapili iliyopita, Zulu pamoja na umahiri wake wa kucheza vema eneo lake la kiungo sambamba na Thaban Kamusoko, alifunga bao ambapo katika ushindi wa mabao 5-1 Yanga iliposhinda dhidi ya Ngaya De Mbe.

“Ni jambo jema kufunga bao tena mchezo wa kwanza wa kimataifa, naamini imeniongezea kitu ndani yangu, zaidi ni kushukuru muunganiko mzuri wa timu kupambana kupata matokeo,” alisema kiungo huyo.

Alisema taratibu ameanza kuingia kwenye mfumo wa kocha George Lwandamina na atazidi kufanya makubwa huko mbele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here