Home Burudani ‘ZUNGUSHA SNURA’ HADHARANI SEPT. 16

‘ZUNGUSHA SNURA’ HADHARANI SEPT. 16

453
0
SHARE

NA GLORY MLAY
MSANII wa filamu nchini, Snura Mushi, amesema anatarajia kufanya uzinduzi wa wimbo wake mpya wa ‘Zungusha Snura’, aliomshirikisha msanii Christian Bella, ambao utafanyika katika ukumbi wa Maisha Basement, jijini Dar es Salaam.
Snura ameliambia DIMBA kwamba, uzinduzi huo utafanyika Septemba 16, mwaka huu, ambapo miongoni mwa wasanii watakaomsindikiza usiku wa shoo atakuwapo msanii Roma Mkatoliki.
“Natarajia kuzindua video ya wimbo wangu mpya ambao nimemshirikisha Bela, nawaambia wadau wangu wajitokeze kwa wingi kushuhudia ‘Live’ snura akizungusha kiuno chake matata, pia kutakuwa na wasanii wakali, akiwamo Roma na wengine waliopata mwaliko,” alisema.
Alisema kutakuwa na shindano la kumtafuta mkali wa kuzungusha kiuno kati ya Kinyama Sina na Matukunyema na atakayebahatika kushinda ataondoka na zawadi nono.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here