SHARE


LIVERPOOL wametakiwa kutoa kitita cha pauni milioni 61, ili kufanikisha uhamisho wa kiungo wa Benfica na timu ya Taifa ya Ureno ya vijana wenye umri wa chini ya mika 21, Joao Felix.

Thierry Henry anamtaka Fellaini Monaco

KOCHA wa Monaco, Thierry Henry, amesema anahitaji kumsajili kwa mkopo kiungo Mbelgiji, Marouane Fellaini, mwenye umri wa maika 31 kutoka  Manchester United.

Maurizio Sarri anasaka kiungo

WAKATI Chelsea wakiwa katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Gonzalo Higuain kutoka Juventus, kocha wa The Blues, Maurizio Sarri, bado yuko bize sokoni kusaka saini ya kiungo, ingawa hajaweka wazi jina lake.

Bayern Munich watuma ofa Chelsea

BAYERN Munich wametuma ofa Chelsea kumvuta winga, Callum Hudson-Odoi. Mkataba wa kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 ndani ya The Blues unamwezesha kupokea pauni 85,000 kwa wiki.

Martial akubali kuongeza miaka mitano Man Utd

STRAIKA wa Manchester United Mfaransa, Anthony Martial (23), amekubali kuongeza mkataba mwingine  wa miaka mitano kuendelea kuhudumu ndani ya mashetani hao wekundu.

Pochettino hana mpango na Rossi

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema hana mpango wa kumsajili mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anaichezea Genoa, Giuseppe Rossi, tofauti na ilivyokuwa inaelezwa.

Everton nao watua kwa Batshuayi

EVERTON pia wamejitosa katika mbio za kumuwinda straika Mbelgiji, Michy Batshuayi, ambapo tayari wametenga mezani pauni milioni 40 kumchomoa Valencia anakocheza kwa mkopo, huku mabosi wake wakiwa nao Chelsea.

Wachina waweka dau mezani kumchomoa Arnautovi West Ham

GUANGZHOU Evergrande ya China, tayari wameweka wazi ofa yao ya pauni milioni 35 kupata uhamisho wa Marko Arnautovic kutoka West Ham United.

Wolves wavuta subira hadi majira ya kiangazi

WOLVES wanasubiri hadi hapo majira ya kiangazi ndipo wamalizane na Benfica kumsajili moja kwa moja straika, Raul Jimenez, mwenye umri wa miaka 27 ambapo thamani yake ni pauni milioni 30.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here