SHARE

MANCHESTER, England

YUPO mtu mmoja aliwahi kusema jambo pekee ambalo analipenda ni kumpatia kazi mtu mvivu, kwa sababu anaamini mvivu atatafuta njia rahisi ya kufanya kazi ngumu.

Mtazame kwa umakini Scott McTominay alivyo sasa. Itazame miguu yake inavyofanya kazi maradufu zaidi ya alivyokuwa katika kikosi cha wachezaji wa akiba.

Kuna vitu vingi vimejificha kwenye miguu ya McTominay, ilikuwa rahisi kwa Warren Joyce wakati yupo na kikosi cha vijana kubainisha kile kilicho bora katika miguu na akili ya mchezaji huyo mrefu.

“Scottni mchezaji mzuri sana, alivyokuja alikuwa tofauti na hivi sasa ni kiungo mzuri ambaye hana mambo mengi, anatambua kazi yake anapokuwa uwanjani,” alisema Joyce.

Baadaye ilibainika kuwa McTominay alikuwa moja ya wachezaji wavivu sana katika mazoezi kiasi cha kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha vijana, huku muda mwingi akizitumikia dakika 30 za mwisho.

Ilikuwa changamoto kubwa sana kwake, hususani katika kipindi ambacho alikuwa anatumiwa katika nafasi tofauti huku ikiaminika kwa umbo lake refu anaweza kucheza kama mshambuliaji. Mara kadhaa alionekana kumudu nafasi hiyo na kufunga mabao.

Historia yake inavutia sana lakini maisha yake ya uwanjani yanavutia zaidi, kwa sababu ndipo anapo lijenga jina lake kwa sasa. Wakati macho ya Louis van Gaal yanaona ufanisi wa kazi wa Marcus Rashford na vijana wengine 13, hayaku bahatika kuona nini kilikuwepo kwenye miguu ya McTominay.

Mlangowa bahati haukumpitia mbali tena, macho ya Jose Mourinho yalimwona nakushawishika na uwezo wake hususani pale alipoamuru jina la mchezaji huyol iongezwe katika orodha ya wachezaji watakao kwenda Marekani kwenye ‘preseason’.

Hakuhitaji nafasi nyingine ya kuthibitisha ubora wake zaidi ya kucheza michezo miwili kwa kiwango cha juu tena katika eneo la kiungo ambalo hakuonekana kucheza sana wakati yupo timu ya vijana.

Pamoja na uvivu aliowahi kuwa nao nadhani aliamini ile ilikuwa nafasi sahihi kwake kumwonyesha Mourinho uwezo wake. Baada ya kuhojiwa na MUTV, McTominay alisema: “Mimi na Rashford tumecheza wote wakati tuna miaka 16. Kupandishwa kwake timu kubwa kulinifanya nijitume nikiamini ipo siku nitapata nafasi, lakini kuwepo katika kikosi huku Marekani ni wazi kocha ameniamini.”

Wapo wanaoamini McTominay ni mrithi sahihi wa Michael Carrick, inawezekana ikawa hivyo japo ni mapema sana kumtabiria mafanikio hayo.

Hana uwezo mkubwa kama Paul Pogba lakini amekuwa akifanya kazi yake kwa ufasaha zaidi, huku mara nyingi akionekana kutimiza majukumu ambayo anapewa naMourinho.

“Scottni mchezaji mzuri sana, mchezaji wa kisasa katika eneo la kiungo, anafanya kila kitu. Kitu pekee ambacho bado hajafanya ni kufunga mabao, japo naamini anaweza. Jambo pekee linalomfanya asifunge inatokana na majukumu ambayo nampa,” alisemaMourinho baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea msimu uliopita.

Haikuonekana kuwa kazi rahisi kwa McTominay kumfanya Eden Hazard acheze mbali na goli la Manchester United, jambo ambalo liliwaweka wakina Chris Smalling na Victor Lindelof katika utulivu mkubwa. Lakini kwa upande mwingine alikuwa kiunganishi mzuri wa mashambulizi ya timu hiyo hasa bao la pili lililofungwa na Jesse Lingard kwa krosi nzuri ya Romelu Lukaku.

Kwa muda mfupi ameishinda imani ya Mourinho kwa kutimiza majukumu yote anayopewa nakocha huyo. Lakini kitu pekee kilicho mshawishi mchezaji huyo kupata nafasi kwenye kikosi cha Man United ni urefu alionao.

Mourinho ni muumini wa wachezaji wenye maumbo makubwa, McTomiany ana urefu wa futi 6 na inchi 4 sawa na Nemanja Matic, huku akizidiwa nusu inchi na Maroune Fellaini.

Dhidi ya Sevilla alikuwa na kazi moja tu ya kukata mawasiliano kati ya Ever Banega na Steven Nzonzi, kwa kiasi kikubwa aliifanya kazi hiyo vizuri na kukivuruga kiungo cha Sevilla ambacho kilibadili mbinu na kupitia kwa ma winga wao kuanzisha mashambulizi.

McTominay wa kesho atakuwa katika mazingira gani? Endapo majeraha yatampita mbali atakuwa mchezaji mkali zaidi ya sasa, sababu atakuwa na uzoefu maradufu wa kupambana na kuhakikisha timu inapata ushindi katika uwepo wake ndani ya uwanja.

Pia maendeleo ya ubora wake ilitegemea na usajili ambao utafanywa na Mourinho ilikulinda nafasi yake katika kikosi cha kwanza, japo mara kwa mara kumekuwa natetesi za timu hiyo kusajili kiungo mwingine.

Lakini Mourinho amefukuzwa ndani ya klabu hiyo, nafasi yake imechukuliwa na Ole GunnarSolskjaer ambaye hivi karibuni alisema atahakikisha kila mchezaji anapata muda wa kucheza na kufurahia mpira.

Kwa maana hiyo, McTominay kama atafanya vizuri ndani ya kikosi hicho kwa muda huo wa Solskjaer atakuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya Manchester United.

Maisha yake ya kesho yapo mikononi mwake mwenyewe kuendelea kuishi katika ubora wake ambao ulimfanya Mourinho abadili maswali kuhusu Pogba kuwa McTominay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here