SHARE

LONDON, England

MKUU wa benchi la ufundi la Tottenham, Mauricio Pochettino, ataamua hatima yake klabuni hapo mara tu itakapomalizika mechi yao ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool.

Spurs na Liverpool zitakwaana Juni mosi huko Hispania baada ya kuziondoa Ajax na Barcelona katika hatua ya nusu fainali.

Pochettino alikuwa akihusishwa kwenda Manchester United na Real Madrid, lakini kwa sasa PSG, Bayern Munich na Juventus ndizo zinazotajwa.

“Ni ngumu kwangu kuelezea (hatima). Ni mazungumzo yangu na Daniel (Levy, Mwenyekiti wa Tottenham), natakiwa kumsikiliza. Yeye ndiye bosi, ndiye mmiliki,” alisema kocha huyo.

Aidha, Pochettino aliwamwagia sifa wachezaji wake kwa kitendo cha kupindua meza dhidi ya Ajax, ambapo katika mchezo wa kwanza walichapwa bao 1-0, kabla ya kushinda 3-2 wakiwa ugenini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here