SHARE

MANCHESTER, ENGLAND

STRAIKA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester United, Sergio Aguero, ameonekana kuwa chachu ya kikosi hicho kutetea taji hilo baada ya kufanikiwa kufunga hat-trick, katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Huddersfiel Town.

Muagentina huyo alikuwa anasahihisha makosa aliyoyafanya mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Arsenal, timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo alikuwa amekosa nafasi za wazi tatu.

Hat-trick hiyo ilikuwa inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo msimu huu ukiwa ni mchezo wa pili kwa timu zote 20 za ligi hiyo inayotajwa kufuatiliwa kwa idadi kubwa zaidi na ulimwenguni kote.

Ilikuwa ni ha-trick yake ya tisa kwenye ligi hiyo pekee akishabihiana na straika wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler, huku kinara akiwa ni Alan Shearer aliyeitumikia katika timu za Newcastle United na Blackburn Rovers kwa nyakati tofauti.

Makali ya mfungaji  huyo wa muda wote wa Manchester City kuhitimisha wikiendi kwa kitisho inamfanya kufunua ukurasa wa kutambua mambo makubwa matano.

 

Avuruga timu za vijana

Straika huyo mwenye uwezo wa kutumia vizuri miguu yote miwili kipaji chake kilianza kuonekana kushawishi timu kubwa kuwania saini yake akiwa na umri wa chini ya miaka 20.

Akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina ya vijana wenye umri huo, alifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu mashindano ya Olimpiki, kabla ya kutwaa ubingwa wa dunia na 2005 na 2007.

Hat-trick ya ubingwa Premier League

Mkali huyo aliyejiunga na Man City 2011 akitokea Atletico Madridm amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England, 2011/2012, 2013/2014 na 2017/2018.

Mbali na mataji hayo, lakini pia Aguero amenyanyua makombe ya ligi mawili, 2013/2014, 2015/2016 pamoja na 2017/2018 pamoja na Ngao ya Jamii 2012 na 2018.

Amjibu Tevez

Kitendo cha kutwaa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora msimu wa 2014/15 akiingia wavuni mara 26, alikuwa amemjibu Muagentina mwenzake, Carlos Tevez.

Tevez alikuwa mchezaji wa kwanza Muagentina wa kwanza kuwa mfungaji bora kwenye ligi hiyo, 2010/2011 akifunga mabao 20 hapo hapo katika kikosi cha Manchester City.

SHARE
Previous articleJAMAI RAJA
Next articleYANGA YAVAMIA KIGALI KIBABE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here