SHARE

BIRMINGHAM, England


KLABU ya Aston Villa imemfuta kazi mkurugenzi wake wa michezo, Jesus Garcia Pitarch, ambaye kimsingi ndiye aliyehusika katika usajili uliogharimu mkwanja mrefu, Pauni milioni 140 (zaidi ya Sh bil. 410 za Tanzania).

Sehemu ya wachezaji waliosajiliwa na Mhispania huyo ni Mbwana Samatta, sambamba na Trezeguet, Wesley, Bjorn Engels, Frederic Guilbert na Marvellous Nakamba.

Lawama juu yake ni kwamba kiasi cha fedha kilichotumika ni kikubwa kuliko mchango wa wachezaji aliowasajili, hivyo hana budi kuwajibika kwa kuondoka klabuni hapo.

Uamuzi wa kumtimua Pitarch unakuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Villa iliponusurika kuiaga Ligi Kuu ya England katika siku ya mwisho ya mechi za kumaliza msimu huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here