SHARE

NA ABDULAH MKEYENGE

ANKO Ngassa ametoa kauli iliyowachekesha wengi. Amemwambia kiungo mkabaji wa timu ya Azam FC na timu ya taifa Tanzania, Mudathir Yahaya, kuwa watakutana Misri kwenye michuano ya Mataifa Afrika ambako Tanzania imefuzu kushiriki michuano hiyo.

Ngassa ametoa kauli hiyo baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga na Azam FC na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na bao hilo likifungwa na Ngassa mwenyewe.

Kauli hiyo ya Ngassa itamfanya kocha wa Stars, Emmanuel Amunike, kummulika kiungo huyo mkongwe katika kikosi chake cha wachezaji 23 watakaokwenda Misri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here