SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MPENZI wa msanii wa Bongofleva Ben Pol, aitwaye Anerlisa amesema licha ya kufurahia mahusiano yao lakini amekua akikumbana na changamoto mbalimbali.

Anerlisa raia wa Kenya amesema mahusiano yake yamedumu kwa muda sasa huku akiyafurahia lakini miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni wanawake kumsumbua mpenzi wake sambamba na muda mwingi kuhitaji kuwa pamoja.

ìNafurahi mahusiano yetu yanaendeelea kuwa imara kadri muda unavyokwenda, changamoto hazikosekani kubw aikiw ani sumbufu wa hapa na pale wa wanawake, hii hasa inachangiwa na kazi yake lakini napambana, pia muda mwingi inanibidi niwe nayeîalisema Anerlisa.

Hata hivyo mwanadada huyo alisema, anatambua kila mahusiano lazima yakumbane na changamoto hivyo anachukulia kama sehemu ya kurutubisha penzi lao.Wawili hao ambao muda mwingi wapo nchini Kenya inadaiwa tayari wamefunga ndoa ya kimya kimya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here