SHARE

LONDON, ENGLAND

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang , hajashtushwa na taarifa za timu hiyo kutaka kumuuza beki Shkodran Mustafi, nyota huyo ameshindwa kujizuia na kujikuta akilike ujumbe uliowekwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram ukimuhusisha staa kutakiwa na Monaco.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani alijiunga na miamba hiyo ya Londoni mwaka 2016 kwa dau la Euro milioni 35.

Inashangaza nyota huyo alizomewa na mashabiki wa Arsenal alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Calum Chambers, katika mchezo ambao washika bunduki walilala dhidi ya Lyon.

Mashabiki wa Arsenal wanaonyesha kuwa hawataki kuendelea kumuona Mustafi huku gazeti la L’Equipe likiripoti kuwa Monaco wanamtaka mlinzi huyo wa kati.

Beki huyo mwenye miaka 27 amekuwa akipambana kuhakikisha anapata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu alipotua katika Ligi kuu ya England, Arsenal wameripotiwa kuwa wapo tayari kumuachia staa huyo kwa dau la Euro milioni 30.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here