SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA kutoka kiwanda cha Bongomovie Aunty Ezekiel amewataka watu wanaofuatilia maisha yake ya mahusiano wamuache afanye yake anayojisikia kwani hawajui magumu anayopitia.

Hivi karibuni Aunty Ezekiel alirudiana na baba mtoto wake Mose Iyobo ambaye inadaiwa kwa sasa wameachana tena na sasa yupo kwenye mahusiano na mtu mwingine.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Aunty alisema amekua akipitia changamoto nyingi za mahusiano hivyo ni vyema watu wasimuhukumu kwa lolote.

“Nasikia yanayoendelea mitandaoni,ukweli ningependa watu wasizungumzie mahusiano yangu kwa sasa nawaomba sana”alisema Aunt.

Aidha Aunty ameongeza kuwa kipindi hiki amekua akitumia muda kukaa nyumbani kwake na akijiweka mbali zaidi na marafiki kutokana na janga la covid 19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here