SHARE

NA MOHAMED KASSARA

HATIMAYE timu ya Azam FC imefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kushinda michezo saba mfululizo ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Ihefu FC mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa jana Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mabao yaliyowapa Wanalamba lamba hao yaliwekwa kambani na Ayoub Lyanga dakika ya 55 na Iddi Seleman ‘Nado’ aliyepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Ihefu FC.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi zake 21 na kuwatimulia vumbi washindani wake Simba na Yanga wanaofukuzia kwa kasi.

Azam FC pia imeweka rekodi ya kucheza michezo sita bila kuruhusu wavu wake kuguswa

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit ‘Zaka za Kazi’ alisema wanapambana kuhakikisha wanashinda  kila mchezo ili kutimiza lengo lao la kutwa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Kikubwa kwasasa ni kuona kwamba kila siku tunapata matokeo mazuri na kuendelea kuweka rekodi kwani hakuna timu ambayo haipendi kupata matokeo mazuri,” alisema Zaka za Kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here