SHARE

MAREGES NYAMAKA NA ABDUL MKEYENGE


WADHAMINI wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanaorusha matangazo hayo moja kwa moja, Azam Televisheni,  wametenga  tiketi 250  kwa mashabiki ili kushuhudia mchezo wa watani wa jadi, Simba dhidi ya Yanga.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa  usiku wa Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, huku matangazo yakianza kurushwa na kituo hicho kuanzia asubuhi.

Akizungumza na waandishi  wa habari, Mkurugenzi wa masoko wa Azam Media, Abdul Mohamed, alisema hicho ni kitu kipya kitakachoongeza thamani ya ‘dabi’  hiyo kubwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Namna pekee ya kupata tiketi hizo kwa wateja wetu kushuhudia mchezo huo ni kulipia miezi mitatu kifurushi cha Play ambacho malipo yake ni Sh 28,000 kwa mwezi,” alisema.

Kwa upande wa mkuu wa vipindi wa Azam Media, Baruan Muhuza, alisisitiza mchezo huo kupitia runinga utakuwa na mwonekano bora maradufu huku kila mfanyakazi akifanya kazi kwa weledi wa juu hasa upande wa kamera.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here