SHARE

NA JESCA NANGAWE

BAADA ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea nchini Rwanda, benchi la ufundi la Azam FC limetamba kwamba watahakikisha wanatetea ubingwa wao.

Akizungumza na Dimba, kocha Mkuu wa kikosi hicho Etienne Ndayiragije, alisema vijana wake wapo tayari kwa mapambano, lengo likiwa ni kufanya kweli na kurudi Dar es Salaam na ubingwa.

“Michuano hii ni migumu kwani timu zote shiriki zinaonekana kujiandaa vizuri. Tunamshukuru Mungu kwamba tumefika hatua ya robo fainali na kilichopo ni kupigana kiume tutetee ubingwa wetu,” alisema.

Kikosi hicho cha Azam FC kimewasili jijini Kigali, Rwanda jana Jumamosi saa 7 mchana, tayari kwa mechi ya robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Kagame wiki ijayo.

Azam FC imetokea mjini Huye, Rwanda ilipokuwa ikicheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kabla ya juzi Ijumaa kufuzu kwa robo fainali ikiwa na KCCA ya Uganda katika Kundi B.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here