SHARE

LAGOS, Nigeria

BENSON Idonije, ambaye ni babu wa mwanamuziki mwenye jina kubwa Nigeria, Burna Boy, amemtabiria ushindi wa tuzo ya Grammy mjukuu wake huyo.

Burna Boy ameingia kwenye orodha ya wasanii wa Nigeria waliowahi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hizo kubwa, akiungana na wakongwe King Sunny Ade, Femi Kuti na Seun Kuti.

Kwa mujibu wa mzee Idonije, ni zamu ya mjukuu wake kuibeba katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo itakayofanyika mwakani, licha ya kushindanishwa na wakali Angelique Kidjo, Altin Gun, Bokante & Metropole Orkest, Nathalie Joachim na Spektral Quartets.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here