SHARE

LONDON, England

MPACHIKAJI mabao mkongwe, Dimitar Berbatov, amewaambia Chelsea wasidhani staa wao mpya, Timo Werner, anaweza kuwapa ubingwa msimu ujao.

Berbatov alisema usajili wa Mjerumani huyo ni mwanzo mzuri lakini si kwamba huduma yake inaweza kuifanya Blues iwe moja kati ya timu zenye ubora wa Liverpool.

Chelsea walimtangaza nyota huyo Alhamisi ya wiki hii, wakimng’oa RB Leipzig kwa dau la Pauni milioni 47.5.

“Chelsea wamempata lakini nafikiri bado wana safari ndefu kuwa timu ya kuwania ubingwa. Yeye si (Lionel) Messi wala (Cristiano) Ronaldo…” alisema Berbatov aliyewahi kupita Tottenham na Manchester United.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here