SHARE

NA MWANDISHI WETU

HAMU ya wapenzi wa timu ya Simba ni kumuona uwanjani straika wao, John Bocco, aliyekosekana kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Bocco aliumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, mechi iliyochezwa Agosti 17, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuonekana majeraha yake yanachukua muda mrefu, uongozi wa klabu ya Simba uliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa vipimo zaidi.

Bocco tayari amerejea nchini na jana alitinga katika mazoezi ya timu hiyo akifanya mazoezi ya pamoja na wenzake katika gym ya Hoteli ya Golden Tulip.

Mkali huyo wa mabao ambaye ni nahodha wa kikosi hicho, alionekana yuko fiti tofauti na alivyokuwa katika mazoezi ya nyuma, alipokuwa anafanya pekee yake.

Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, alisema Bocco alirudi juzi kutoka Afrika Kusini, wanasubiri awakabidhi ripoti ya daktari wa huko ili waone jinsi ya kumpangia majukumu.

@@@@@@@@@@

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here