SHARE

NA MWANDISHI WETU

ALIYEKUWA Rais wa Klabu ya Yanga, Abbas Tarimba,amejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Tarimba jana alitinga Ofisi za chama hicho Wilaya ya Kinondoni na kuchukua fomu kuomba kugombea nafasi ya ubunge.

Tarimba alifika katika ofisi za CCM Kinondoni Mkwajuni,saa mbili asubuhi akiwa pekee na kuchukua fomu na kisha kuirejesha saa tatu kamili asubuhi.

Mara baada ya kurudisha fomu Tarimba alisema,anaamini ni muda muafaka kwake kuwatumikia wakazi wa Kinondoni baada ya kujitathimini kabla ya kuchukua uamuzi wa kugombea nafasi iyo.
Alisema, anafahamu changamoto zote za wilaya hiyo kutokana na kuwahi kuwa Diwani wa Kata ya Hannanasifu, Kinondoni kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia 2005 -2015.

ìMimi hapa Kinondoni siyo mgeni, nipo hapa ninaishi kwa muda mrefu hivyo ninajua kitu gani ambacho wanakitaka wakazi wa wilaya hii kikubwa niwawahidi mengi makubwa,îalisema Tarimba ambaye ni Mkurugenzi Uwekezaji wa SportPesa Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here