SHARE

NA TIMA SIKILO

KIPA wa kimataifa Mtanzania David Kissu,anayecheza soka la kulipwa nchini Kenya katika klabu ya Gor Mahia,amesema amemis kucheza soka la nyumbani.

Kissu ambaye alijiunga na Gor Mahia Julai 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, anayafurahia maisha ndani ya klabu hiyo lakini ameanza kukumbuka bongo.

Kauli ya mchezaji huyo imekuja huku kukiwa na taarifa kuwa hana maelewano na mabosi wa Gor Mahia kutokana na kuidai klabu hiyo mamilioni ya pesa za malimbikizo ya mishahara yake.

“Nimelimis soka la nyumbani lakini ndo hivyo bado nina mkataba na Gor Mahia ingawa napitia kwenye changamoto ya kufanya kazi bila kulipwa kwani ninawadai malimbikizo ya pesa zangu nyingi,”alisema
Inaelezwa nyota huyo mbioni kuvunja mkataba na klabu hiyo kama hatolipwa fedha zake anazowadai.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here