SHARE

LAGOS, Nigeria


STAA wa muziki, David Adeleke ‘Davido’, ameingia makubaliano na Serikali ya Jimbo la Rivers na kazi yake itakuwa ni kuibua na kuendeleza vipaji katika eneo hilo.

Mbali ya kutembelea miradi kadhaa ya maendeleo, Davido alimtaja Gavana wa Jimbo hilo, Nyesom Ezenwo Wike, kuwa ni kiongozi anayetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, Davido alitumia nafasi hiyo kutangaza tamasha lake kubwa litakalofanyika Port Harcourt Desemba, mwaka huu, akiweka wazi kuwa mbali ya wasanii wa Nigeria, pia wanamuziki wa nje watapanda jukwaani ‘kukiwasha’.

“Tumepania kuwawezesha vijana. Kuwasaidia wanamuziki kufikia mafanikio ndiyo lengo,” alisema msanii huyo bilionea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here