SHARE

MANCHESTER, England

DAVID de Gea hana hofu ya kupoteza nafasi yake ya chaguo la kwanza katika lango la Manchester United, licha ya kiwango kibovu katika siku za hivi karibuni.

Makosa mengi, yakiwamo yaliyoifanya Man United ifungwe na Chelsea katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA, yalitishia usalama wa nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza.

Mbaya zaidi, kipa wa United aliyekuwa na Sheffield United kwa mkopo, alikuwa bora msimu uliopita, hivyo De Gea kutabiriwa kupoteza namba mbele ya Muingereza huyo.

“Najiamini,” alisema De Gea na kuongeza: “Nimeonesha ubora wangu kwa miaka yote, hivyo bado nina nafasi kwa kocha.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here