SHARE

NA VICTORIA GODFREY

MSANII wa Bongo Flava nchini Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz anatarajia kutoa burudani katika pambano la kuwania mkanda wa Mabingwa wa Mabara (IBA), kati ya bondia Mfaume Mfaume dhidi ya raia wa Ufilipino, Arney Tinampay.

Pambano hilo la raundi 12 la uzito wa 69 ambalo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika litafanyika Agosti mwaka huu,Uwanja wa Uhuru, jijini hapa.

Promota wa Ngumi za Kulipwa, Jay Msangi, alisema, mazungumzo yanaendelea kufanyika na msanii huyo ili aweze kutoa burudani katika pambano hilo.

Tuanaendelea na mazungumzo na Platnumz na yanaendelea vizuri hivyo tunaimani atakubali ombi letu ili aweze kuwasindikiza mashabiki wake, alisema Msangi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here