SHARE

Na CHARLES MULLINDA –

aliyekuwa Dubai

KATIKA mkutano huo wa Dubai, David Abraham ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Studio ya Wonderhood ya nchini Uingereza, naye alipata fursa ya kuwasilisha mada kuhusu kuelekea mwisho wa kulipia vipindi vya televisheni.

Kama Dotse, Abraham naye alialikwa na Kampuni ya MultiChoice,  kutoa mada ya kutoa uzoefu wake kwa wahariri na maofisa  habari  hao kuhusu matumizi ya mitandaoya kijamii.

Akiwasilisha mada yake, Abraham alisema watoa huduma wa mitandao ya kijamii katika Afrika, bado wana fursa nyingi za utafutaji wa maudhui miongoni mwa watumiaji na watazamaji wa mitandao hiyo barani Afrika.

Kwa kurejea uzoefu wake wa miaka mingi wa kuwajengea uwezo wahariri wa vipindi vya televisheni, filamu, waandishi wa habari za uchunguzi, siasa, vichekesho, michezo ya kuigiza na matukio mbalimbali, alisema ingawa ni vigumu kutabiri hali ya usoni itakuwaje katika matumizi ya mitandao Afrika, bado kuna fursa nyingi za utafutaji wa maudhui miongini mwa watazamaji wa mitandao ya kijamii katika Bara la Afrika.

“Bara la Afrika na vijana wake, pamoja na matumizi ya simu za mkononi, vinaweza kuongeza masoko kwa upande wa Magharibi kwa ajili ya manufaa ya baadaye,” alisema Abraham.

Akichangia uzoefu wake katika shughuli za mitandao ya kijamii barani Ulaya, alisema baadhi ya maeneo yanayofanya vizuri nchini Uingereza, Bara la Ulaya kwa ujumla na hata Marekani ni malipo ya vipindi vya televisheni na kwamba hilo liliwezekana kutokana na majadiliano yaliyofanywa na wadau wa mitandao kwa ajili ya siku za baadaye za matumizi ya mitandao.

Alisema katika Bara la Ulaya na Marekani, ukuaji wa masoko mitandaoni unazidi kuwa mkubwa na hivyo kutishia biashara ya vipindi vya televisheni na katika matumizi ya mitandao na kwamba  kuna uzingatiaji wa kila athari ya muda mrefu kutokana na teknolojia pamoja na mifumo ya baadaye katika malipo ya televisheni na usambazaji wake.

Abraham alisema, awali kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya huduma za bure za televisheni na watoa huduma ambao walikuwa wanatengeneza mazingira ya kulipwa kutokana na maudhui.

“Wakati huo, watoa huduma za simu nao walikabiliana na ushindani katika jukwaa la maudhui, ili kujenga uaminifu kwa wateja na haki katika ulimwengu, ushindani wa kimataifa wa kidigitali ulizidi kuongezeka na kuwa tishio katika ulimwengu wa teknolojia,” alisema Abraham.

Hata hivyo, Abraham alisema swali moja ambalo linabaki bila majibu kwa sasa lakini huenda likapa majibu huko mbeleni ni namna gani watumiaji mitandao katika Afrika watakuwa na uwezo wa kuwafikia watoa huduma mbalimbali ili kupata maudhui bora zaidi yatayosaidia kazi za kiafrika kuwavutia wengi.

Alisema kwa uzoefu wake wa kuendesha vipindi vya televisheni katika nchi za Ulaya na Marekani kuanzia mwaka 2001 hadi 2017, mazingira ya maudhui na huduma yamekuwa yakibadilika kila mara na kwa Afrika, bado kuna fursa pana zaidi ya kusaka maudhui kwa kazi za kiafrika zinazoandaliwa na waafrika wenyewe.

Kwamba haina shaka tena katika siku za usoni vipindi vya televisheni vitakavyokuwa vikilipiwa vitapungua kwa kadri matumizi ya dijitali yanavyoendelea kushika kasi kulingana na uboreshaji wa mazingira ya usambazaji wa intaneti katika sehemu mbalimbali za Afrika.

ABRAHAM

Abraham ni mmoja wa watu wanaoheshimika zaidi katika ulimwengu wa kidijitali.

i Mkurugenzi Mkuu wa Wonderhood Studios na kwa muda wa miaka 30 amefanya kazi kama kiongozi katika studio na televisheni mbalimbali, biashara na ubunifu nchini Uingereza na Marekani.

Kutokana na uzoefu wake, ameshiriki mikutano na makongamo mengi ya kimataifa kama mtendaji maarufu wa vyombo vya habari mbalimbali.

Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Channel 4, mwaka 2010 hadi 2017, alipata umaarufu mkubwa baada ya kuwa kiongozi wa muda mrefu wa channel hiyo aliyeweza kurudisha hadhi ya kituo hicho kutokana na ubunifu wake uliowezesha kuandaliwa kwa vipindi bora vilivyokubaliwa na umma.

Ni katika kipindi hicho cha uongozi ndani ya

Channel 4, aliweza kuvumbua njia ya mabadiliko makubwa ya kidigitali kwa kujenga mkakati wa data ambao leo hii una watumiaji zaidi ya milioni 15 nchini Uingereza unaojulikana kwa jina la All4.

Abraham ni mmoja wa wataalamu waliohusika katika kueneza matumizi ya digitali nchini Uingereza na Bara la Ulaya mwaka 2000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here