SHARE

MADRID, Hispania


BAADA ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kutia mguu kwenye mikikimikiki ya La Liga, nyota wa Real Mallorca, Luka Romero, amekuwa akifananishwa na Lionel Messi.

Hata hivyo, Romero aliyeweka rekodi hiyo alipoingia uwanjani akiwa na umri wa miaka 15 na siku 219, alisema: “Inanikera kufananishwa naye kwa sababu kuna Messi mmoja tu na nataka kuweka jina langu kwenye soka nikiwa kama Luka Romero.”

Kwa upande mwingine, nyota huyo wa kimataifa wa Mexico alifichua alikotokea akisema wazazi wake ni raia wa Argentina, hivyo yeye ana uraia wa nchi tatu, ikiwamo Hispania.

Aliongeza kuwa anaweza kucheza moja kati ya mataifa hayo katika siku za usoni lakini angefurahi zaidi kufanya kazi na kikosi cha Argentina kwa kuwa hata baba yake alikuwa mwanasoka nchini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here