SHARE


NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA Faiza Ally amefunguka kuwa mara baada ya kuona mzazi mwenzie Joseph Mbilinyi amefunga ndo aliangusha kilio kikali ili kuonyesha hisia zake za kuumizwa na jambo hilo.


Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini alifunga ndoa hiyo Jumamosi iliyopita katika Kanisa Katoliki la Ruanda Mkoani Mbeya na mchumba wake Happynes Msonga.


Akizungumza na DIMBA Jumatano,Faiza alisema, kitendo cha kufunga ndoa kwa baba mtoto huyo hakikua kigeni kwa kuwa tayari alishapewa taarifa bali alitaka kuonyesha hisia zake kwake kwa kuwa bado anampenda.


“Watu watambue mimi napenda kulia na baada ya kulia moyo wangu umekua na amani sana, kwa sasa na waombea ndoa njema na nitajisikia vibaya kuona ndoa hiyo inaingia kwenye matatizo kwa kwa nachoamini natamani kuwaona wanafika mbali kwa kuwa hata mimi nimesharidhika na hali iliyotokea”alisema Faiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here