SHARE

 Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa Hip hop, Fareed Kubanda maarufu Fid Q ameuanza mwaka 2019 kitofauti baada ya kukamilisha matukio makubwa mawili ndani ya siku mbili tofauti.

Tukio la Kwanza alilofanya Desemba 31 ni kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi anayemwita kwa jina la ‘Mama Cheusi’.

Na tukio la pili amramua kufunga ndoa, Januari Mosi na huyo ‘Mama Cheusi’ wake. Sherehe ya harusi yao ilihudhuliwa na mastaa wa fani mbalimbali wakiwemo msanii mwenzake, Ambwene Yessaya (AY). Ay ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza ndoa hiyo baada ya kutuma ujumbe na picha katika ukurasa wake wa Instagram akimpongeza Fid Q kwa hatua hiyo.

“Hongera sana ndugu yangu kwa kufunga ndoa,mwenyezi Mungu aibariki ndoa yenu, ” aliandika AY.

Baada ya matukio hayo mashabiki na wasanii wenzake wengine wamemtuma salama za pongezi pamoja na kumtakia kheri katika ndoa yao hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here