SHARE

NA JESSCA NANGAWE

SIKU chache baada ya mrembo kutoka Bongofleva Gigy Money kumwagana na mpenzi wake Hancho raia wa Nigeria amekiri kuwa ni wazi sasa anaumizwa na mapenzi.

Gigy Money ambaye amekua kwenye mahusiano tofauti miaka ya nyuma amesema si kwamba hapendi kudumu kwenye mahusiano bali amekua akikutana na watu ambao wanamuumiza.

“Hakuna ambaye hapendi maisha ya amani,,mimi nikipenda najitoa kwa kila kitu lakini ukinivuruga naacha mazima,sipendi kuona nanyanyasika au nadharauliwa na mpenzi wangu,ukweli naumizwa sana”alisema Gigy.

Hata hivyo mrembo huyo amekiri kuwa sababu kubwa ya kutofautiana na mpenzi wake huyo ni malumbano ya hapa na pale ambayo hakuweza kuyavumilia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here