SHARE

PARIS, UFARANSA

Klabu ya Paris Saint Germain, imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Senegal na klabu ya Everton, Idrisa Gana Gueye na kumpa kandarasi ya miaka minne huku dau lake likiwa siri.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alijiunga na Everton akitokea Aston Villa tangu alipotua katika dimba la Goodson Park alicheza jumla ya michezo 108.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa, wamemnasa staa huyo ili kwenda kuziba pengo la Adrien Rabiot, ambaye ameondoka katika kikosi hicho na kutua Juventus kama mchezaji huru.

Tayari ‘Toffees’ wathibitisha kuwa hawatakua na nyota huyo msimu ujao wa Ligi Kuu ya England na  hivi sasa wameanza kusaka mbadala wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here