SHARE

NA JESSCA NANGAWE

ZIARA ya staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul maarufu kama Harmonize, imemalizika nchini Marekani huku akitamba kumletea mafanikio makubwa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, meneja wa msanii huyo, Joel Vincent, alisema ziara yao ambayo ilihitimishwa Oktoba 20 ilibebwa na idadi kubwa ya mashabiki waliofurika kushuhudia burudani.

“Nashukuru tumemaliza salama ziara yetu ilikuwa na mafanikio makubwa, kwani mbali ya kujipatia mashabiki wengi lakini pia imetupa mwanga zaidi na tumefanikiwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wasanii ambao wanatamani kufanya kazi na Harmonize,” alisema Joel.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here