SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII Rajab maarufu kama Harmonize anatarajia kutambulisha wasanii watatu wapya mapema mwezi ujao kupitia lebo yake mpya ya Konde Music World wide.
Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu staa huyo amtambulishe msanii Ibra ambaye kwa sasa anafanya vyema chini ya lebo hiyo.

Akizungumza na DIMBA,Harmonize alisema,wasanii hao watatangazwa rasmi Agosti mwaka huu ambapo wataungana na kuendelea kufanya mapambano makubwa katika lebo hiyo.

ìKwanza nipende kutangaza kuwa mashabiki wajiandae na ujio wa wasanii wengine ambao natarajia kuwatangaza kazi rasmi mwezi ujao, hii itakua sehemu ya mipango yetu katika kuendeleza kurudumu la muziki wetuîalisema Harmonize.

Hata hivyo aliongeza kuwa moja ya mipango mikubwa ndani ya lebo hiyo ni kufanya kazi na wasanii wenye uwezo mkubwa ambao wataipa heshima kubwa lebo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here