SHARE
Eden Hazard,

MADRID, Hispania

RASMI staa wa timu ya Real Madrid, Eden Hazard, hataonekana katika mashindano ya Supercopa de Espana yanayotegemewa kufanyika nchini Saudi Arabia mwaka huu, akiendelea kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu.

Madrid itaivaa Valencia katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo na itakutana na mshindi kati ya Barcelona na Atletico Madrid katika fainali ya mashindano hayo.

Majeraha yamekuwa ni kikwazo kwa Mbelgiji huyo tangu atue Santiago Bernabeu akitokea Chelsea. Msimu huu amecheza mechi nane za La Liga, akifunga bao moja tu na kukosa mtanange wa El Clasico.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here