SHARE
Jacob Steven JB

BEATRICE KAIZA

MSANII wa Filamu Jacob Steven JB amesema kuwa ameweka historia ya kuwa binadamu mwenye uzito mkubwa kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo tukio hilo limemfungilia njia ya kupata nafasi ya kushiriki kwenye Twenzetu Ki-Nature.

Akizungumza na DIMBA,JB alisema,kuwa amepata nafasi hiyo kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kupanda Mlima Kilimanjaro na sasa amepata nafasi nyingine ya watu wachache ambao wataoshiriki.

ëíNimeweka historia ya kuwa binadamu mwenye uzito mkubwa kupanda Mlima Kilimanjaro ambapo nimepata nafasi nyingine tena ya kushiriki kwenye Twenzetu Ki- Nature ambayo inahusisha ziara kwenye maeneo 17 ambayo yana uoto wa asili kama Tanga, Bagamoyo, Meru, Same, Kalambo Waterfall na msitu wa Pugu,íí alisema JB.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here